Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عن أبي هريرة رضي الله عنه قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: «قَالَ اللهُ تَبَارَكَ وَتَعَالَى: أَنَا أَغْنَى الشُّرَكَاءِ عَنِ الشِّرْكِ، مَنْ عَمِلَ عَمَلًا أَشْرَكَ فِيهِ مَعِي غَيْرِي تَرَكْتُهُ وَشِرْكَهُ».
Tafsiri
Imepolelewa Kutoka kwa Abuu Huraira -Radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: amesema: Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake-: "Amesema Allah aliyetakasika na kutukuka: Mimi nimetosheka (sihitaji) washirika kushirikishwa nao, yeyote mwenye kufanya jambo akashirikisha ndani yake mwingine pamoja nami, nitamuacha na ushirika wake".
Ufafanuzi
Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka amesema kuwa: Yeye amejitosheleza na uhitaji wa washirika wa kushirikishwa naye, Yeye ni tajiri wa kila kitu, na kuwa mwanadamu atakapofanya jambo katika ibada na akalifanya kuwa ni la Mwenyezi Mungu na mwingine asiyekuwa yeye, basi Allah humuacha na halikubali jambo hilo, na hulirejesha kwa mwenye nalo. Ni lazima kutakasa amali kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, kwani Yeye Mtukufu hakubali isipokuwa yale yatakayokuwa yametakaswa kwa kutaka radhi zake Yeye Mkarimu.
Mafunzo
- Tahadhari ya ushirikina kwa aina zake zote; nakuwa ushirikina huzuia kukubaliwa amali.
- Kuleta hisia ya utajiri wa Allah na utukufu wake ni katika mambo yanayosaidia kutakasa matendo.
Ufafanuzi: العربية
يُخبِرُ النبيُّ صلى الله عليه وسلم أنَّ الله تبارك وتعالى قال بأنه أغنى الشركاء عن الشرك، فهو الغني عن كل شيء، وأنَّ الإنسانَ إذا عَمِل عملًا من الطاعات وجَعَلَه لله ولغير الله؛ تَركَه اللهُ ولم يقبلْه منه، وردَّه على صاحبِه؛ فيجبُ إخلاصُ العمل لله تعالى؛ لأنه سبحانه لا يَقبل إلا ما كان خالصًا لوجهِه الكريم.
- التحذير من الشرك بجميع أشكاله، وأنه مانعٌ من قبول العمل.
- استشعار غنى الله وعظمته مما يعين على الإخلاص في العمل.