Hadithi

Atakayekuja miongoni mwenu kwa ajili ya Ijumaa basi na aoge

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عن عَبْدِ اللهِ بْنِ عُمَرَ رضي الله عنهما قَالَ: سَمِعْتُ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ: «‌مَنْ ‌جَاءَ ‌مِنْكُمُ ‌الْجُمُعَةَ فَلْيَغْتَسِلْ».

Tafsiri

kutoka kwa Abdullahi bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Nilimsikia Mtume rehema na amani ziwe juu yake akisema: "Atakayekuja miongoni mwenu kwa ajili ya Ijumaa basi na aoge".

Ufafanuzi

Anasisitiza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa atakayetaka kuja kwa ajili ya swala ya Ijumaa basi inapendeza kwake kuoga, mfano wa kuoga kwake josho la janaba.

Mafunzo

  • Mkazo wa kuoga kwa ajili ya Ijumaa, nakuwa hilo ni sunna kwa muumini siku ya Ijumaa na ikiwa wakati anataka kwenda kuswali ndio bora zaidi.
  • Kutilia manani swala la usafi na harufu nzuri ni katika tabia njema za muislamu na adabu zake, na amri inakuwa na mkazo zaidi wakati wa kukutana na watu na kukaa nao, hasa hasa katika mikusanyiko na swala za jamaa.
  • Tamko katika hadithi linamuhusu mwenye uwajibu wa kuswali Ijumaa; kwa sababu yeye ndiye anayekwenda kuswali.
  • Ni lazima kwa mwenye kwenda katika swala ya Ijumaa awe msafi, aoge ili harufu iondoke katika mwili wake na ajitie manukato, na ikiwa atatawadha pekee pia itatosha.
Ufafanuzi: العربية

يُؤَكِّدُ النبيُّ صلى الله عليه وسلم على مَن أراد أنْ يأتي لصلاة الجمعة فإنه يستحب له أن يغتسل، مثل غُسلِه للجنابة.

  • تأكيد غُسْل الجمعة، وأنه سنة للمؤمن يوم الجمعة وأنْ يكون عند الذهاب للصلاة أفضل.
  • الحرص على النظافة وطيب الرائحة من أخلاق المسلم وآدابه، ويتأكد الأمر عند مُلاقاة الناس ومجالستهم، لا سيما في الجمع والجماعات.
  • الخطاب في الحديث لِمَن تَجب عليه الجمعة؛ لأنه هو الذي يأتيها.
  • يستحب لمن يأتي الجمعة أن يكون نظيفًا، فيغتسل حتى تزول الروائح من جسده ويتطيب، وإن توضأ فقط أجزأه ذلك.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi