Hadithi

"Hivi mnajua kuwa Mola wenu amesema nini?" Wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wanajua zaidi, akasema: "Watu wangu kwenye kuteremka Mvua wamegawanyika makundi mawili kuna waumini na makafiri

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ زَيْدِ بْنِ خَالِدٍ الجُهَنِيِّ رضي الله عنه أَنَّهُ قَالَ: صَلَّى لَنَا رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ صَلَاةَ الصُّبْحِ بِالْحُدَيْبِيَةِ عَلَى إِثْرِ سَمَاءٍ كَانَتْ مِنَ اللَّيْلَةِ، فَلَمَّا انْصَرَفَ أَقْبَلَ عَلَى النَّاسِ، فَقَالَ: «هَلْ تَدْرُونَ مَاذَا قَالَ رَبُّكُمْ؟» قَالُوا: اللهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ، قَالَ: «أَصْبَحَ مِنْ عِبَادِي مُؤْمِنٌ بِي وَكَافِرٌ، فَأَمَّا مَنْ قَالَ: مُطِرْنَا بِفَضْلِ اللهِ وَرَحْمَتِهِ، فَذَلِكَ مُؤْمِنٌ بِي وَكَافِرٌ بِالْكَوْكَبِ، وَأَمَّا مَنْ قَالَ: بِنَوْءِ كَذَا وَكَذَا، فَذَلِكَ كَافِرٌ بِي وَمُؤْمِنٌ بِالْكَوْكَبِ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Zaid Bin Khalid Aljuhaniy -Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Alitusalisha Mtume wa Mwenyezi Mungu -Rehema na amani ziwe juu yake- Sala ya Asubuhi katika mji wa Hudaibiyah wakati mvua iliponyesha usiku, na alipomaliza akawageukia watu na kuwauliza: "Hivi mnajua kuwa Mola wenu amesema nini?" Wakasema: Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wanajua zaidi, akasema: "Watu wangu kwenye kuteremka Mvua wamegawanyika makundi mawili kuna waumini na makafiri, Basi yeyote atakayesema tumenyeshelezewa Mvua kwa fadhila za Mwenyezi Mungu basi huyo ni mwenye kuniamini mimi, na ni mwenye kuupinga unajimu, ama atakayesema kuwa tumenyeshelezewa Mvua kwa sababu ya nyota fulani na fulani, basi huyo amenikadhibisha mimi na kaziamini nyota."

Ufafanuzi

Aliswali Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- sala ya Asubuhi katika mji wa Hudaibiyah- nacho ni kijiji kilichopo karibu na Makkah, baada ya kunyesha Mvua usiku. Na alipomaliza sala yake aliwageukia watu kwa kuwaelekea, akawauliza: Hivi mnajua alichosema Mola wenu Mtukufu? Basi wakajibu kuwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake ndiyo wajuzi zaidi, Akasema: Kwa hakika Mwenyezi Mungu ameeleza kuwa watu wamegawanyika makundi mawili wakati wa kuteremka Mvua, kuna kundi ni lenye kumuamini Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kundi lingine ni lenye kumkufuru Mwenyezi Mungu Mtukufu; Basi atakayesema tumenyeshelezewa kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na rehema zake, na akaegemeza kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu suala la kushuka mvua; Basi huyo ni mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu muumba mwenye kuendesha ulimwengu, na ni mwenye kupinga unajimu. Ama atakayesema: Tumenyeshelezewa mvua kwa sababu ya Nyota fulani; Basi mtu huyo ni kafiri, na ni mwenye kuamini nyota -unajimu- na kufuru ndogo ikiwa kuteremka mvua kutaegemezewa kwenye kutazamia Nyota; Na Mwenyezi Mungu hakuzifanya Nyota kuwa sababu ya kunyesha mvua na wala hakupanga iwe hivyo, Na ama atakayeegemeza suala la kuteremka mvua na matukio mengine ya Ardhini kwenye mzunguko wa Nyota wakati wa kuchomoza kwake na kuanguka kwake ya kuwa ndiyo kisababishi cha hakika, basi mtu huyo amekufuru kufuru iliyokubwa,

Mafunzo

  • Ni sunna kusema baada ya kuteremka Mvua: Tumenyeshelezewa Mvua kwa fadhila za Mwenyezi Mungu na Rehema zake.
  • Yeyote atakaye egemezea neema ya kuteremka Mvua na neema zingine katika Nyota kwa kuumbwa na kuwepo kwake basi mtu huyo ni kafiri aliyekufuru kufuru kubwa, ama yule atakayeegemeza kuwa Nyota ni sababu basi huyo amekufuru kufuru ndogo, kwa sababu Nyota siyo sababu ya kuteremka mvua kisheria wala kihisia.
  • Nikuwa neema inakuwa ni sababu ya kukufuru endapo itakanushwa, na huwa ni sababu ya kuwa na imani endapo itashukuriwa.
  • Kumekatazwa kusema kuwa: "Tumepata mvua kwa kuanguka Nyota fulani" hata kama yatakuwa makusudio yake ni wakati fulani (kama msimu wa masika); kwa kuzuia mlango wa shirki.
  • Ni wajibu kuufungamanisha moyo na Mwenyezi Mungu Mtukufu, katika kuleta neema na kuondosha matatizo.
Ufafanuzi: العربية

صلى النبي صلى الله عليه وسلم صلاة الصبح بالحديبية -وهي قرية قريبة من مكةـ بعد مطر نزل في تلك الليلة، فلما سلم وانتهى من صلاته أقبل على الناس بوجهه، فسألهم: هل تدرون ماذا قال ربكم عز وجل؟ فأجابوه: الله ورسوله أعلم، فقال: إن الله تعالى بَيًّن أن الناس ينقسمون عند نزول المطر إلى قسمين: قسم مؤمن بالله تعالى، وقسم كافر بالله تعالى؛ فأما من قال: مطرنا بفضل الله ورحمته، ونَسَب إنزال المطر إلى الله تعالى؛ فذلك مؤمن بالله الخالق المتصرف في الكون، وكافر بالكوكب. وأما من قال: مطرنا بنجم كذا وكذا؛ فذلك كافر بالله، مؤمن بالكوكب، وهو كفر أصغر حيث نسب إنزال المطر إلى الكوكب؛ والله لم يجعله سببًا شرعيًا ولا قدريًّا، وأما من نسب نزول المطر وغيره من الحوادث الأرضية إلى تحرُّكات الكواكب في طلوعها وسقوطها معتقدًا أنها الفاعل الحقيقي، فهو كافر كفرًا أكبر.

  • استحباب القول بعد نزول المطر: مُطرنا بفضل الله ورحمته.
  • من نسب نعمة إنزال المطر وغيرها إلى الكوكب خَلْقًا وإيجادًا فهو كافرٌ كفرًا أكبر، وإن نسبه على أنه سببٌ فهو كافرٌ كفرًا أصغر لأنه ليس بسبب شرعي ولا حسي.
  • أن النعمة تكون سببًا للكفر إذا كُفِرت، وتكون سببًا للإيمان إذا شُكرت.
  • النهي عن قول: "مطرنا بنوء كذا"، ولو قُصِد بها الوقت؛ سدًّا لذريعة الشرك.
  • وجوب تعلُّق القلب بالله تعالى في جَلْب النعم ودفع النقم.
  • هذا الحديث مما يرويه النبي صلى الله عليه وسلم عن ربه، ويسمى بالحديث القدسي أو الإلهي، وهو الذي لفظه ومعناه من الله، غير أنه ليست فيه خصائص القرآن التي امتاز بها عما سواه ، من التعبد بتلاوته والطهارة له والتحدي والإعجاز وغير ذلك.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi