Hadithi

Nilikuwa nikimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitoa salamu kuliani kwake, na kushotoni kwake, mpaka ninaona weupe wa shavu lake

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa Imamu Muslim

Matini ya Kiarabu

عَنْ سَعْدٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ قَالَ: كُنْتُ أَرَى رَسُولَ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُسَلِّمُ عَنْ يَمِينِهِ، وَعَنْ يَسَارِهِ، حَتَّى أَرَى بَيَاضَ خَدِّهِ.

Tafsiri

Kutoka kwa Sa'd radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Nilikuwa nikimuona Mtume rehema na amani ziwe juu yake akitoa salamu kuliani kwake, na kushotoni kwake, mpaka ninaona weupe wa shavu lake.

Ufafanuzi

Ameeleza Sa'di bin Abii Waqasi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba alikuwa akiona shavu la Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutokana na kugeuka kwake sana anapotoa salamu kwa ajili ya swala yake, kuliani kwake kwa ajili ya salamu ya kwanza, na kushotoni kwake kwa ajili ya salamu ya pili.

Mafunzo

  • Sheria ya kupitiliza katika kugeuka katika upande wa kulia na upande wa kushoto.
  • Sheria ya kutoa salamu mbili kuliani na kushotoni.
  • Amesema Nawawi: Na lau mtu atatoa salamu mbili kuliani kwake au kushotoni kwake au mbele yake au ya kwanza kushotoni kwake na ya pili kuliani kwake swala yake itakuwa sahihi, lakini atakosa fadhila ya usahihi wake.
Ufafanuzi: العربية

أخبر سعد بن أبي وقاص رضي الله عنه أنه كان يرى بياض خدِّ النبي صلى الله عليه وسلم من شدة التفاتِهِ إذا سلَّم من صلاته عن يمينه للتسليمة الأولى، وعن يساره للثانية.

  • مشروعية المبالغة في الالتفات إلى جهة اليمين وإلى جهة اليسار.
  • مشروعية التسليمتين إلى اليمين واليسار.
  • قال النووي: ولو سلَّم التسليمتين عن يمينه أو عن يساره أو تلقاء وجهه أو الأولى عن يساره والثانية عن يمينه صحت صلاته وحصلت التسليمتان، ولكن فاته الفضيلة في كيفيتهما.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi