Hadithi

Lilikuwa tandiko la Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kutokana na ngozi, na ndani limejazwa majani ya mitende

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: كَانَ فِرَاشُ رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مِنْ أَدَمٍ، وَحَشْوُهُ مِنْ لِيفٍ، وَلِمُسلمٍ: كَانَ وِسَادَةُ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ الَّتِي يَتَّكِئُ عَلَيْهَا مِنْ أَدَمٍ حَشْوُهَا لِيفٌ.

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Lilikuwa tandiko la Mtume rehema na amani ziwe juu yake ni kutokana na ngozi, na ndani limejazwa majani ya mitende, na katika riwaya ya Muslim: ulikuwa mto wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliokuwa akiegamia umetokana na ngozi ndani umejazwa majani.

Ufafanuzi

Ameeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuwa godoro alilokuwa akilalia Mtume rehema na amani ziwe juu yake lilikuwa limetengenezwa kwa ngozi, na limejazwa majani ya mitende, na vile vile mto wake aliokuwa akiegemea.

Mafunzo

  • Kumebainishwa hali aliyokuwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake kama vile kuipa nyongo dunia na kuzipuuza ladha za dunia, pamnoja nakuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu alimpa uwezo wa hilo lau kama angetaka kustarehe nayo.
  • Inafaa kutumia magodoro na mito, na kuvilalia na kuwa juu yake.
  • Muislamu anatakiwa kuzingatia hali yake na hali ya maisha ya Nabii wake rehema na amani ziwe juu yake. Kwani yeye ndiye kiigizo chema, na kwamba mwenye kuiga nyenendo zake ataongoka na atafaulu duniani na Akhera.
  • Kuwa na pupa ya kuiandaa Akhera, na muumini atosheke katika dunia na kile kinachomsaidia katika kumtii Mwenyezi Mungu, na asishughulike na kutafuta wingi wa mali ndani yake, na aliwakemea Mwenyezi Mungu watu, akasema: "Kumekupumbazeni kutafuta wingi (wa mali) mpaka mkayazuru makaburi" [Takathur: 1-2].
Ufafanuzi: العربية

أخبرت أم المؤمنين عائشة رضي الله عنها أن الفراش الذي كان ينام عليه رسول الله صلى الله عليه وسلم مصنوع من جلد مَدْبوغ، ومملوء بليف من النخل، وكذلك مخدته التي يستند عليها.

  • بيان ما كان عليه النبي صلى الله عليه وسلم من الزهد والإعراض عن ملاذ الدنيا، مع أن الله سبحانه وتعالى مكَّنه من ذلك لو شاء أن يستمتع بها.
  • جواز اتخاذ الفرش والوسائد، والنوم عليها والارتفاق بها.
  • ينبغي للمسلم أن يعتبر حالَه ومعيشتَه بحال نبيه صلى الله عليه وسلم، فإنه الأسوة الحسنة، وأن من اقتفى آثاره اهتدى وأفلح في الدنيا والآخرة.
  • الحرص على الإعداد للآخرة، وأن يكتفي المؤمنُ من الدنيا بما يُعينه على طاعة الله، وألا يُشغل بالتَّكاثر فيها، وقد ذمَّ الله قومًا فقال: {أَلْهَاكُمُ التَّكَاثُرُ حَتَّى زُرْتُمُ الْمَقَابِرَ} [التكاثر:1- 2].

Mada

Ripoti kosa

Zaidi