Hadithi

(Shikamaneni na) Swala nyinyi na waliomilikiwa na mikono yenu ya kuume

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiImepokelewa na Nasai katika kitabu Alkubraa na Ibn Majah

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَنَسٍ رَضيَ اللهُ عنه قَالَ: كَانَتْ عَامَّةُ وَصِيَّةِ رَسُولِ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ حِينَ حَضَرَهُ الْمَوْتُ: «الصَّلَاةَ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ، الصَّلَاةَ وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ»، حَتَّى جَعَلَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يُغَرْغِرُ بِهَا صَدْرُهُ، وَمَا يَكَادُ يُفِيضُ بِهَا لِسَانُهُ.

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Anas radhi za Mwenyezi Mungu ziwe ju yake amesema: Ulikuwa usia mkubwa wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alipofikwa na mauti: "(Shikamaneni na) Swala nyinyi na waliomilikiwa na mikono yenu ya kuume, (Shikamaneni na) Swala nyinyi na waliomilikiwa na mikono yenu ya kuume", mpaka akaanza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kushikwa na kwikwi kifuani kwake kwa maneno hayo kwa sababu ya kifo, na maneno hayo yalikaribia kujaa ulimi wake.

Ufafanuzi

Ulikuwa usia mwingi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa Umma wake naye akiwa katika ulevi wa kifo: Shikamaneni na swala na mdumu nayo na wala msighafilike nayo, na vile vile timizeni haki za wale wanaomilikiwa na mikono yenu ya kuume miongoni mwa watumwa na wajakazi na wamilikini kwa wema, akaendelea kuukariri, mpaka ukaanza kumkwama katika koo lake, na ulimi wake ukashindwa kuutamka kwa ufasaha.

Mafunzo

  • Ukubwa wa jambo la swala na haki ya mamluki; kwa sababu Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliusia mambo hayo mawili katika mwisho wa yale aliyousia.
  • Swala ni katika haki kubwa za Mwenyezi Mungu kwa waja wake, na kutimiza haki za viumbe na hasa hasa madhaifu, nao ni wale waliochini ya mkono wa mtu wasiokuwa kizazi chake nalo ni katika haki kubwa za viumbe.
Ufafanuzi: العربية

كانت أكثر وصية النبي صلى الله عليه وسلم لأمته وهو في سكرات الموت: إلزموا الصلاة وحافظوا عليها ولا تغفلوا عنها، وكذا أدوا حقوق ما ملكت أيمانكم من العبيد والإماء وأحسنوا ملكتهم، فما زال يكررها، حتى جعل يُغَرْغِر بها حلقُه، وما يكاد يفصح بها لسانه.

  • عظم شأن الصلاة وحق ملك اليمن؛ لأن النبي صلى الله عليه وسلم أوصى بهما في آخر ما أوصى.
  • الصلاة من أعظم حق الله على عباده، وأداء حق الخلق وخاصة الضعفة ومن هم تحت اليد من غير الذرية من أعظم حقوق الخلق.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi