Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عن عبد الله بن عكيم رضي الله عنه مرفوعاً: «مَنْ تَعَلَّقَ شيئا وُكِلَ إليه».
Tafsiri
Kutoka kwa Abdillah bin Hakim- Radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake- Hadithi Marfu'u: "Mwenye kukitegemea kitu hufungamanishwa kwacho".
Ufafanuzi
Atakayegeuka kwa moyo wake au vitendo vyake au kwa vyote viwili katika kitu ambacho anataraji manufaa au kuzuia madhara, Mwenyezi Mungu humuwakilisha katika kitu hicho ambacho amekielekea, atakayemuelekea Mwenyezi Mungu humtosheleza na humfanyia wepesi kila zito, na mwenye kumuelekea asiyekuwa yeye Mwenyezi Mungu humfungamanisha katika kitu hicho na humfedhehesha.
Mafunzo
- Katazo la kuegemea kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu.
- Ulazima wa kuegemea kwa Mwenyezi Mungu katika mambo yote.
- Kubainishwa madhara ya ushirikina na ubaya wa mwisho wake.
- Malipo huendana na matendo.
- Nikuwa malipo ya kitendo hurudi kwa mfanyaji yakiwa ya kheri au ya shari.
- Kushindwa kwa mwenye kujiondoa kwa Mwenyezi Mungu na akatafuta manufaa kwa asiyekuwa yeye.
Ufafanuzi: العربية
من التفت بقلبه أو فعله أو بهما جميعا إلى شيء يرجو منه النفع أو دفع الضر وكله الله إلى ذلك الشيء الذي تعلَّقه، فمن تعلَّق بالله كفاه ويسَّر له كل عسير، ومن تعلق بغيره وكله الله إلى ذلك الشيء وخذله.
- النهي عن التعلق بغير الله -تعالى-.
- وجوب التعلق بالله في جميع الأمور.
- بيان مضرة الشرك وسوء عاقبته.
- أن الجزاء من جنس العمل.
- أن نتيجة العمل ترجع إلى العامل خيرا أو شرا.
- خذلان من انصرف عن الله وطلب النفع من غيره.