Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0
Matini ya Kiarabu
عَنْ أَبِي مُوسَى رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَامَ فِينَا رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بِخَمْسِ كَلِمَاتٍ، فَقَالَ: «إِنَّ اللهَ عَزَّ وَجَلَّ لَا يَنَامُ، وَلَا يَنْبَغِي لَهُ أَنْ يَنَامَ، يَخْفِضُ القِسْطَ وَيَرْفَعُهُ، يُرْفَعُ إِلَيْهِ عَمَلُ اللَّيْلِ قَبْلَ عَمَلِ النَّهَارِ، وَعَمَلُ النَّهَارِ قَبْلَ عَمَلِ اللَّيْلِ، حِجَابُهُ النُّورُ -وَفِي رِوَايَةٍ: النَّارُ- لَوْ كَشَفَهُ لَأَحْرَقَتْ سُبُحَاتُ وَجْهِهِ مَا انْتَهَى إِلَيْهِ بَصَرُهُ مِنْ خَلْقِهِ».
Tafsiri
Kutoka kwa Abuu Mussa radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Alisimama kwetu Mtume rehema na amani ziwe juu yake kwa maneno matano, akasema: "Hakika Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu na Mtukufu, halali, na wala haimstahikii kulala, hushusha mizani ya uadilifu na huinyanyua, yanapandishwa kwake matendo ya usiku kabla ya matendo ya mchana, na matendo ya mchana kabla ya matendo ya usiku, pazia lake ni nuru, -na katika riwaya nyingine-: Lau kama angeliondoa, basi utukufu wa uso wake ungeunguza viumbe vyake mpaka pale ambapo macho yake yanafikia."
Ufafanuzi
Alisimama Mtume rehema na amani ziwe juu yake akihutubia kwa Maswahaba zake kwa sentensi tano kamilifu, nazo ni: Ya kwanza: Kuwa Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka halali. Ya pili: Haiwezekani katika haki yake kulala; kulingana na ukamilifu wa usimamizi wake na uhai wake. Ya tatu: Ya kwamba Yeye Mtukufu anashusha mizani na kuinyanyua kulingana na vile vinavyopimwa miongoni mwa matendo ya waja yanayopanda kwake juu, na zinapimwa riziki zao zinazoshuka katika Ardhi, riziki ambayo ndiyo sehemu na fungu la kila kiumbe huishusha Yeye Mtukufu na kumfanya awe masikini, na huipandisha na kumfanya awe tajiri. Ya nne: Hupandishwa kwake waliyoyafanya waja usiku kabla ya mchana unaofuata baada yake, na amali zao za mchana kabla ya amali za usiku unaofuata baada yake; Malaika wanaohifadhi matendo ya waja hupanda na matendo ya usiku baada ya kumalizika kwake katika mwanzo wa mchana, na wanapanda na amali za mchana baada ya kumalizika kwake katika mwanzo wa usiku. Ya tano: Pazia lake Mtukufu linalozuia kumuona ni nuru au moto, laiti angelifunua basi mwangaza wa uso wake ungeunguza kila kitu mpaka pale linapoishia jicho lake katika viumbe vyake; mwangaza wa uso wake ni nuru yake na utukufu wake na mng'ao wake. Na makadirio: Nikuwa, lau angeliondoa na kukifunua kinachozuia kumuona ambacho ni pazia, na akajitokeza wazi nuru ya uso wake ingeliunguza kila kitu mpaka linapoishia jicho lake katika viumbe vyake; navyo ni viumbe vyote; kwa sababu jicho lake Aliyetakasika na kutukuka limezingira viumbe vyote.
Mafunzo
- Kumebainishwa kutowezekana kulala kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu; kwakuwa hilo ni katika mapungufu, na yeye ametakasika na hayo.
- Mwenyezi Mungu Mtukufu anamtukuza amtakaye na anamdhalilisha amtakaye, na anamuongoza amtakaye na anampoteza amtakaye katika waja wake.
- Matendo hunyanyuliwa kwa Mwenyezi Mungu kila mchana na usiku, na katika hilo kuna himizo kwa waja wamchunge Mwenyezi Mungu Aliyetakasika na kutukuka katika usiku wao na mchana wao.
- Hadithi inaonyesha uadilifu wa Mwenyezi Mungu Mtukufu na uzuri wa upangiliaji wake wa mambo ya viumbe wake, na hakuna shaka kuwa hii ni katika sifa za ukamilifu wake Aliyetakasika na kuwa juu.
- Kumethibitishwa pazia lake Aliyetakasika na kutukuka, nayo ni nuru inayokinga baina yake na baina ya viumbe wake, na lau isingekuwa hiyo wanageliungua.
- Amesema Aajurri: Hakika watu wa haki humsifu Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kile alichojisifu mwenye Mtukufu, na kwa kile alichomsifu nacho Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake, na kwa kile walichomsifia Maswahaba radhi za Allah ziwe juu yao, na huu ndio msimamo wa wanachuoni katika wale walioamua kufuata sheria na hawakuzusha. Mwisho wa kunukuu. Watu wa sunna (wanaofuata mafundisho ya Mtume) wanamthibitishia Mwenyezi Mungu kile alichojithibitishia yeye mwenyewe katika majina na sifa, pasina kupotosha wala kukanusha wala kuuliza namna yake wala kupiga mfano, na wanamkanushia Mwenyezi Mungu yale aliyoyakanusha kwake, na wananyamaza kwa yale ambayo hayakukanushwa wala kuthibitishwa, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: "Hakuna kitu kama mfano wake, na Yeye ni msikivu mwenye kuona".
- Nuru ambayo ndiyo sifa yake Aliyetakasika na kutukuka si nuru ambayo amejikinga nayo, nuru aliyojikinga nayo imeumbwa, nuru ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni nuru inayoendana naye Yeye na dhati yake, hakuna kitu kama mfano wake, na alichokiona Mtume rehema na amani ziwe juu yake hakikuwa kingine zaidi ya pazia linalokuwa kati ya Mwenyezi Mungu na waja wake.
Ufafanuzi: العربية
قام النبي صلى الله عليه وسلم خطيبًا في أصحابه بخمس جملٍ تامة، وهي: الأولى: بأن الله عز وجل لا ينام. الثانية: يستحيل في حقه النوم؛ لكمال قيوميته وحياته. الثالثة: أنه تعالى يخفض الميزان ويرفعه بما يوزن من أعمال العباد المرتفعة الصاعده إليه، ويوزن من أرزاقهم النازلة إلى الأرض، فالرزق الذي هو قسط ونصيب كل مخلوق يخفضه سبحانه فيقتره، ويرفعه فيوسعه. الرابعة: يُرفع إليه ما عمل العباد بالليل قبل النهار الذي بعده، وعملهم بالنهار قبل عمل الليل الذي بعده؛ فالملائكة الحفظة يصعدون بأعمال الليل بعد انقضائه في أول النهار، ويصعدون بأعمال النهار بعد انقضائه في أول الليل. الخامسة: حجابه سبحانه المانع من رؤيته النور أو النار، لو كشفه لأحرقت سبحات وجهه ما انتهى إليه بصره من خلقه؛ فسبحات وجهه نوره وجلاله وبهاؤه. والتقدير: لو أزال وكشف المانع من رؤيته وهو الحجاب، وتجلى لخلقه لأحرقت سبحات وجهه ما انتهى إليه بصره من خلقه؛ وهي جميع المخلوقات؛ لأن بصره سبحانه وتعالى محيط بجميع الكائنات.
- بيان استحالة النوم على الله سبحانه وتعالى؛ لكونه من النقائص وهو منزه عنها.
- الله تعالى يُعزُّ من يشاء ويذل من يشاء، ويهدي من يشاء ويضل من يشاء من عباده.
- الأعمال ترفع إلى الله كل يوم وكل ليلة، وفي ذلك حث للعباد أن يراقبوا الله عز وجل في ليلهم ونهارهم.
- الحديث يدل على عدل الله سبحانه وحسن تدبيره لأمور خلقه، ولا شك أن هذا من صفات كماله جل وعلا.
- إثبات الحجاب له سبحانه وتعالى، وهو النور الحائل بينه وبين خلقه، ولولاه لاحترقوا.
- قال الآجُرِّي: إنَّ أهل الحق يَصِفُون الله عز وجل بما وصف به نفسه عز وجل، وبما وصفه به رسوله صلى الله عليه وسلم، وبما وصفه به الصحابة رضي الله عنهم، وهذا مذهب العلماء ممن اتبع ولم يبتدع. انتهى. فأهل السنة يُثْبِتُون لله ما أثبته لنفسه من الأسماء والصفات من غير تحريف ولا تعطيل ولا تكييف ولا تمثيل، ويَنْفُون عن الله ما نفاه عن نفسه، ويَسْكُتُون عما لم يرد به نفي ولا إثبات، قال الله تعالى: {لَيْسَ كَمِثْلِهِ شَيْءٌ وَهُوَ السَّمِيعُ الْبَصِيرُ}.
- النور الذي هو وصفه سبحانه وتعالى غير النور الذي احتجب به، النور الذي احتجب به نور مخلوق، فنور الله تعالى نور يليق به وبذاته، ليس كمثله شيء، والذي رآه النبي صلى الله عليه وسلم ما هو إلا الحجاب الذي يكون بين الله وبين عباده.