Hadithi

Msiwazuie vijakazi wa Mwenyezi Mungu kwenda katika misikiti ya Mwenyezi Mungu, lakini wakitaka kutoka watoke wakiwa hawajajipamba

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

Ni nzuri (Hasan)Imepokelewa na Abu Daud

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: «لَا تَمْنَعُوا إِمَاءَ اللَّهِ مَسَاجِدَ اللَّهِ، وَلَكِنْ لِيَخْرُجْنَ وَهُنَّ تَفِلَاتٌ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Huraira -radhi za Allah ziwe juu yake- yakwamba Mtume -rehema na amani ziwe juu yake- amesema: "Msiwazuie vijakazi wa Mwenyezi Mungu kwenda katika misikiti ya Mwenyezi Mungu, lakini wakitaka kutoka watoke wakiwa hawajajipamba".

Ufafanuzi

Amemkataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake msimamizi wa mwanamke na muhusika wake kuwakataza wanawake kwenda Msikitini, na akawaamrisha wanawake wakati wa kutoka kwenda Msikitini watoke bila kujipuliza manukato na wasitoke kwa kujiachia kwa mapambo; ili wasiwe sababu ya fitina kwa wanaume.

Mafunzo

  • Kumpa ruhusa mwanamke ya kwenda kuswali Msikitini atapokuwa na uhakika wa kutopata fitina, na akatoka bila mapambo wala manukato.
  • Wameitumia hadithi hii kama ushahidi kuwa mwanamke hatoki nyumbani kwake isipokuwa kwa idhini yake, kwakuwa amri ya idhini imeelekezwa kwa wanaume.
  • Uislamu umewapa kipaumbele wanawake, na kutowazuia kwa mambo ambayo yanaweza kuwa ni heri kwao kama kutoka kwenda kutafute elimu na mfano wake.
  • Kuthibiti kwa usimamizi wa mwanaume juu ya mwanamke na kumchunga.
Ufafanuzi: العربية

نهى النبي صلى الله عليه وسلم ولي المرأة والمسؤول عنها عن منع النساء من المساجد، وأَمَرَ النساء عند الخروج أن يخرجن غير متطيبات ولا متبرجات بزينة؛ حتى لا يكنَّ سببًا في فتنة الرجال.

  • الإذن للمرأة بالصلاة في المسجد إذا أمنت الفتنة، وخرجت بدون زينة ولا طيب.
  • استدل به على أن المرأة لا تخرج من بيت زوجها إلا بإذنه، لتوجه الأمر إلى الأزواج بالإذن.
  • حرص الإسلام على النساء، وعدم منعها مما قد يكون فيه خير لها من الخروج لطلب العلم ونحوه.
  • ثبوت ولاية الرجل على المرأة ورعايته لها.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi