Hadithi

Hawakuwahi kushiba katika chakula cha ngano watu wa famili ya Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake tangu alipofika Madina, kwa siku tatu mfululizo, mpaka alipofariki

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ عَائِشَةَ أُمِّ المُؤْمِنينَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا قَالَتْ: مَا شَبِعَ آلُ مُحَمَّدٍ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ مُنْذُ قَدِمَ المَدِينَةَ مِنْ طَعَامِ البُرِّ ثَلاَثَ لَيَالٍ تِبَاعًا، حَتَّى قُبِضَ.

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Aisha mama wa waumini radhi za Allah ziwe juu yake: Hawakuwahi kushiba katika chakula cha ngano watu wa famili ya Muhammadi rehema na amani ziwe juu yake tangu alipofika Madina, kwa siku tatu mfululizo, mpaka alipofariki.

Ufafanuzi

Anaeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuwa, watu wa nyumba ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake hawakuwahi kushiba tangu walipoingia Madina kwa chakula cha ngano kwa muda wa siku tatu mfululizo, mpaka alipofariki rehema na amani ziwe juu yake.

Mafunzo

  • Kumebainishwa hali aliyokuwa nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya maisha ya chini, kwani maisha halisi ni maisha ya Akhera.
  • Amesema bin Hajari: Na kinachoonekana nikuwa sababu ya kutoshiba kwao mara nyingi ilikuwa ni kwa sababu ya uchache wa upatikanaji wa chochote kwao, yaani walikuwa wakipata chakula lakini walikuwa wakithamini wenye shida zaidi yao kuliko nafsi zao.
Ufafanuzi: العربية

تخبر أم المؤمنين عائشة رضي الله عنها أن أهل بيت النبي صلى الله عليه وسلم لم يشبعوا منذ قدموا إلى المدينة من أكل البُرِّ ثلاثة أيام متتابعات حتى توفي صلى الله عليه وسلم.

  • بيان ما كان عليه النبي صلى الله عليه وسلم وأهله من قلة المعيشة، فإن العيش عيش الآخرة.
  • قال ابن حجر: والذي يظهر أن سبب عدم شبعهم غالبًا كان بسبب قلة الشيء عندهم، على أنهم كانوا قد يجدون ولكن يؤثرون على أنفسهم.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi