Hadithi

Hatokuwa na imani mmoja wenu mpaka yawe matamanio yake ni yenye kufuata yale niliyokujua nayo

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

Amesema Nawawi: Hadithi hii ni sahihiImepokelewa na katika kitabu cha Al-Hujjah kwa msururu sahihi wa wasimulizi

Matini ya Kiarabu

عَنْ أَبِي مُحَمَّدٍ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرِو بْنِ العَاصِ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا، قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: «لَا يُؤْمِنُ أَحَدُكُمْ حَتَّى يَكُونَ هَوَاهُ تَبَعًا لِمَا جِئْتُ بِهِ».

Tafsiri

Imepokelewa kutoka kwa Abuu Muhammadi Abdallahi bin Omari -radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yao- amesema: Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu -rehema na amani ziwe juu yake-: "Hatokuwa na imani mmoja wenu mpaka yawe matamanio yake ni yenye kufuata yale niliyokujua nayo".

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa mwanadam hawezi kuwa muumini mwenye imani kamili ya wajibu mpaka mapenzi yake yafuate yale aliyokuja nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake miongoni mwa amri na makatazo na mengineyo, ayapende aliyoamrishwa, na ayachukie aliyokatazwa.

Mafunzo

  • Hadithi hii ni kanuni ya kujisalimisha katika sheria na kutii.
  • Tahadhari kwa mwanadamu kuwa yeyote mwenye kuipa kipaumbele akili au mazoea na akaitanguliza kuliko yale aliyokuja nayo Mtume rehema na amani ziwe juu yake, basi huyu imani kwake imekanushwa.
  • Ulazima wa kuifanya sheria kuwa ndio muamuzi katika kila kitu, kwa kauli yake: "Yale niliyokuja nayo".
  • Nikuwa imani inaongezeka kwa kumtii Mwenyezi Mungu na inapungua kwa kumuasi.
Ufafanuzi: العربية

بين النبي صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أن الإنسان لا يكونا مؤمنًا كامل الإيمان الواجب حتى تكون محبته تابعة لما جاء به الرسول صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ من الأوامر والنواهي وغيرها، فيحب ما أمر به، ويكْرَهُ ما نَهَى عنه.

  • الحديث قاعدة في التسليم للشرع والانقياد له.
  • تحذير الإنسان من أن من يحكم العقل أو العادة ويقدمه على ما جاء به الرسول صلى الله عليه وسلم، ففاعل ذلك قد نُفي الإيمان عنه.
  • وجوب تحكيم الشريعة في كل شيء، لقوله: «لِمَا جِئتُ به».
  • أن الإيمان يزيد بالطاعة وينقص بالمعصية.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi