Hadithi

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoamka usiku anasafisha kinywa chake kwa mswaki

Chanzo: HadeethEnc.com, Kiswahili v1.18.0

SahihiWamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake

Matini ya Kiarabu

عَنْ حُذَيْفَةَ رضي الله عنه قَالَ: كَانَ النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا قَامَ مِنَ اللَّيْلِ يَشُوصُ فَاهُ بِالسِّوَاكِ.

Tafsiri

Kutoka kwa Hudhaifa -radhi za Allah ziwe juu yake- amesema: Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake anapoamka usiku anasafisha kinywa chake kwa mswaki.

Ufafanuzi

Alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake mara nyingi akipiga mswaki na akiamrisha watu kufanya hivyo, na kuna baadhi ya nyakati kumetiliwa mkazo, mfano; kupiga mswaki wakati wa kuamka usiku, kwani alikuwa rehema na amani ziwe juu yake akisukutua na kutakatisha kinywa chake kwa mswaki.

Mafunzo

  • Mkazo wa sheria ya kupiga mswaki baada ya usingizi wa usiku, kwa sababu usingizi hupelekea mabadiliko ya harufu ya kinywa, na mswaki ndio kifaa cha kusafishia.
  • Mkazo wa sheria ya kupiga mswaki kila wakati wa mabadiliko ya harufu ya kinywa, kwa kuzingatia maana ya awali.
  • Sheria ya usafi kwa ujumla, na kwamba ni sehemu ya Sunna za Mtume rehema na amani ziwe juu yake, na ni katika adabu tukufu.
  • Kupiga mswaki katika kinywa chote kunajumuisha: Meno, fizi, na ulimi.
  • Mswaki ni kijiti kilichokatwa kutoka katika mti wa araki au mti mwingine, na hutumika kusafisha kinywa na meno, na huburudisha kinywa, na kuondoa harufu mbaya.
Ufafanuzi: العربية

كانَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم كثيرًا ما يَستاك ويأمر به، وهو يتأكد في بعض الأوقات، منها: الاستياكُ عند القيام من الليل، حيث كان صلى الله عليه وسلم يَدلُك وينقِّي فاه بالسواك.

  • تأكيد مشروعية السواك بعد نوم الليل، وذلك أنَّ النوم مُقتَضٍ لتَغَيُّر رائحة الفم، والسواك هو آلة تنظيفية.
  • تأكيد مشروعية السواك عند كل تَغَيُّرٍ كريهٍ للفم، أخذًا من المعنى السابق.
  • مشروعية النظافة على وجه العموم، وأنها من سنة النبي صلى الله عليه وسلم، ومن الآداب السامية.
  • التسوُّك في الفم كلِّه يشمل: الأسنان، واللثة، واللسان.
  • السواك هو عُودٌ يُقطَع من شجرة الأراك أو غيرها، ويُستخدم في تنظيف الفم والأسنان، ويطيِّب الفم، ويُزيل الروائح الكريهة.

Mada

Ripoti kosa

Zaidi